PrivChat

Mjadala kuhusiana na teknolojia, haki za binadamu,
na uhuru wa mtandao umeletwa kwako na Tor Project

PrivChat ni mfululizo wa matukio ya harambee yaliyofanywa kuchangia Tor Project. Kupitia PrivChat, tutakuletea taarifa muhimu kuhusiana na nini kinaendelea katika teknolojia, haki za binadamu, na uhuru wa mtandao kwa kukusanya wataalamu wabobezi kuwasilana kwa majibinazo na jamii yetu.

PrivChat kuhudhuria ni bure. Kama umepata thamani toka kwenye matukio haya na umeipenda Tor, tafadhali zingatia kuwa wafadhili wa kila mwezi. Usaidizi wa kutegemewa, unaotabirika ndiyo njia bora ya kuhakikisha Tor inasalia imara na thabiti.

Lengo letu na PrivChat ni kujenga njia mbili za kusaidia. Utapata taarifa kwa kuongoza ufikiriaji nkuhusiana na kufanya kazi katika faragha, teknolojia, na haki za binadamu. Na Tor Project itakuwa na urahisi na kukuwa katika maendeleo yetu kama matokeo ya msaada wako, kuturuhusu sisi kutoa mirejesho kwa wakati ili kuongeza vitisho vya ufuatiliwaji mtandaoni na udhibiti (na kusimamia PrivChats zaidi)!


PrivChat na Tor

Kurasa wa #6- Faragha ni haki ya binadamu

12/15 ∙ 19:00 UTC ∙ 14:00 Eastern ∙ 11:00 Pacific ∙ @torproject YouTube channel

Angalia

Faragha ni kulinda kile kinachotufanya kuwa binadamu: tabia zetu za kila siku, utu wetu, hofu zetu, mahusiano yetu, na kuathirika kwetu. Kila mmoja anastahili faragha. Umoja wa mataifa ulipitisha na kratibu faragha kama haki ya kibinadamu katika Azimio la Ulimwengu la Haki za Kibinadamu mwaka 1948. Hatahivyo, serikali, mashirika, na mamlaka nyingine mara nyingi hutuzuia kutimiza haki yetu ya faragha kwa kufanya ufuatiliaji,kuchukua taarifa na kutudhibiti.

Wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu,walio wachache na watu wanaopinga kuhusu maendeleo mara nyingi hulenga ufuatiliaji huu, hivyo wana mtazamo wa kipekee juu ya umuhimu wa faragha na kutojulikana mtandaoni.

Katika toleo hili la PrivChat, tunawaweka pampja wataalamu wenye uzoefu katika uharakati au kufanya kazi na makundi ya wanaharakati ambao wataongelea uzoefu waloionao katika kufuatilkiwa na faragha:

JiungeAli Gharavi, Mtaalamu mkuu wa Programme, Swedish International Development Agency; Nadya Tolokonnika, wasanii, wanaharakati, na wanachama waanzilishi wa Pussy Riot; naNicholas Merrill, mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji, chu cha Calyx kujadili uzoefu katika ufuatiliaji na kwa nini kupigania faragha ni jambo muhimu katika kuhakikisha haki za binadamu kwa wote.

Cindy Cohn, Mkurugenzi mtendaji wa EFF, atajiunga nasi kama muwezeshaji na msimamizi.

Mtunzaji

Cindy Cohn

Mkurugenzi mtendaji wa, Electronic Frontier Foundation

Cindy Cohn ni mkurugenzi mtendaji wa lectronic Frontier Foundation. Kuanzia mwaka 2000-2015 alitoa kama mkurugenzi wa kisheria wa EFF na mshauri mkuu pia. Mwaka 1993 alitoa huduma kama mwanasheria mkuu wa haki wa Bernstein v. Dept, mafanikio ya changamoto ya marekebisho ya kwanza ya U.S vikwazo vya nje vya kriptographia. Miongoni mwa waheshimiwa wengine , Ms.Cohn alitajwa katika Non Profit Times mwaka 2020 Orodha ya 50 bora ya watu wenye nguvu na ushawishi, Forbes ilihusisha Ms, cohn miongoni wa wanawake 50 bora wa teknolojia wa Marekani. Mwaka 2013, jarida la sheria la kitaifa lilimtaja Ms. Cohn miongoni mwa wanasheria 100 bora wenye ushawishi zaidi Marekani, angalizo "Kama Big Brother anatazama, ni bora amauangalie Cindy Cohn."

Washiriki

Ali Gharavi

Mtaalamu mbobezi mkuu wa progamut, Swedish International Development Agency

Ali Gharavi amekua kiongozi katika uwezeshaji, usauri na usindikizaji wa kimkakati wa taasisi ya watetezi wa haki za binadamu kwa zaidi ya miaka 18 years, na mwandishi mwenza wa usalama wa utafiti-Muongozo wa watetezi wa haki za binadamu. Amesaidia katika kubuni na kutekeleza programu kwa katika kipindi kirefu, uwezeshaji wa taaluma mbalimbali wa taasisi za watetezi wa haki za binadamu kuhakikisha uendelevu na mafanikio yao. Ali aliwezesha, funza na kushauri zaidi ya miradi ya watetezi wa haki za binadamu 2000, taasisi na mashirika na zimefanya kazi kwa uwezo huu zaidi ya nchi 50. Kwa sasa anafanya kama mbobezi mkuu wa programu katika shirika la kimataifa la maendeleo la Sweden (SIDA), Umoja wa Demokrasia na Haki za Binadamu, mkusanyiko wa uhuru wa kujieleza na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Nadya Tolokonnika

Msanii, mwanaharakati, na muasisi wa Pussy Riot

Nadya Tolokonnika ni msamii, mwanaharakati, na muasisi wa Pussy Riot, feministi wa kimataifa anayepinga harakati za sanaa. Pussy Riot inajihusisha na usawa wa kijinsia, ujumuishi, uzazi, upendo, kicheko, machafuko na kupinga ubabe wa mamlaka. Leo hii, utambulisho wa mamia ya watu ni sehemu ya jamii ya Puss Riot. Mwaka 2012, Nadya alifungwa jela miaka 2 kufuatia kupinga utendaji wa Putin na kwenda kwenye mgomo wa kula kupinga hali ya jela na aliishia kupelekwa katika koloni la Siberia, ambako akiweza kudumisha shughuli zake za sanaa na bendi yake ya jela ya Punk ambayo aliiweka pamoja na utalii karibu na kambi ya wafanyakazi wa Siberia. Mwaka 2018, alichapisha kitabu, Read and Riot: Muongozo wa Uharakati wa Pussy Riot. Mwaka 2021, Pussy Riot ilijiunga na PleasrDAO, msaidizi wa uwakilishi wa wanawake kwenye NFT kama mwanachama.

Nicholas Merrill

Muasisi na mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Calyx

Nicholas Merrill Ni muasisi na mkurugenzi wa taasisi ya The Calyx. Awali alianzisha shirika la upatikanaji wa mtandao la Calyx mwaka 1995, mmoja wa mfanyabiashara wa kwanza wa watoa huduma za mtandao lilikuwa linafanya kazi mji wa New York. Kazi zake zimejikita zaidi kutetea haki ya faragha pamoja na uhuru wa kujieleza mtandaoni na katika sekta ya mawasiliano ya simu. Nick alipata tuzo ya ACLU\u2019s Roger Baldwin Medal of Liberty and the Bill of Rights Defense Committee\u2019s Patriot .

Mchango wako unafanya mfululizo huu na kazi zetu katika Tor kuwezekana.

Njia bora ya kuunga mkono kazi zetu ni kuwa mchangiaji wa kila mwezi.

Matoleo

PrivChat na Tor Kurasa wa #5- Ulinzi dhidhi ya wadukuzi

Pamoja na Likhita, Etienne Maynier na John Scott-Railton. Inasimamiwa na Roger Dingledine.

Kila mwaka, serikali, vyombo vya kutekeleza sheria, majeshi na mashirika wanawekeza mabilioni ya dolla katika kutengeneza na kununua programu za udukuzi zilizoundwa kwa lengo la kupenyeza kimyakimya katika kifaa cha mtumiaji na kuwaruhusu washambuliaji kuona maudhio bila kujulikana. Mwaka huu, Mradi wa Pegasus uligungua kuwa watumiaji wa aina hii ya programu inayochunguza taarifa za wengine, wanafahamika kama Pegasus na inaundwa na kundi la NSO, imelenga simu zinazomilikiwa na maelfu wa watu katika nchi zaidi ya 50, ikijumuisha wafanya bishara, wanasiasa, waandishi wa habari, na wanaharakati wa haki za binadamu. Katika toleo hili la PrivChat, jiunge na Likhita na Etienne Maynier wa Amnesty International na John Scott-Railton wa Citizen Lab kujadili namna watu wanaweza kujilinda, taasisi zipi tunaweza zisaidia kuondoa ukiukwaji huu na nani anafanya katika usalama, programu binafsi zaidi tunazoweza ziamini?

PrivChat na Tor Kurasa wa #4- Kumbukizi ya miaka 25 ya Onion Routing

Pamoja na Roger Dingledine, Nick Mathewson, Paul Syverson. Inasimamiwa na Gabriella Coleman.

Sherehekea miaka 25 ya onion routing na Tor! Mei 31, 2021 mi maadhimisho ya miaka 25 ya uwasilishaji wa kwanza katika jamii wa onion routing huko Cambridge, UK katika chuo cha Isaac Newton Institute's Kongamano la kwanzo la kufika Taarifa.

Unakaribishwa kusherekea nyakati hizi muhimu pamoja nasi kuzungumzia uanzishwaji wa onion routing, na namna wazo hili limekuwaTor, na namna Tor Project mwishoni imekuwa. Sisi\u2019ll Tumeungana na Paul Syverson, mmoja wa watunzi wa first onion routing paper, pamoja na waanzilishi wenza wa Tor Project Roger Dingledine and Nick Mathewson.

Tuta akisi katika siku za mwanzo za mtandao wa onion routing network nchini Marekani. Naval Research Lab (NRL). (Hapo nyuma, mawasiliano ya onion router yaliendeshwa kupitia nodes tano badala ya mfumo wa sasa wa Tor unaotumia muundo wa nodes tatu!) Siyo siri kuwa wazo la onion routing lilitokana na NRL (Ipo katika our history page), lakini kuna vitu vya zaidi vingine tunataka kutoa taarifa kuhusiana na namna Tor ilianza na wapi tumetoka katika miaka 25 iliyopita.

PrivChat na Tor Sura ya #3-Tor kuendeleza haki za binadamu

Pamoja na Alison Macrina, Berhan Taye na Ramy Raoof. Inasimamiwa na Ed Snowden.

Dhima kuu ya Tor Project's ni kukuza haki za kibinadamu na uhuru kwa kuunda na kueneza teknolojia huru, za bure na za wazi na faragha na usiri mtandaoni. Watu wanatumia teknolojia yetu, inayoitwa mtandao wa Tor na Tor Browser, kwa njia tofauti. Tor inatumika na watoa taarifa wanaohitaji njia salama kuleta taarifa nzuri za matendo mabaya -- taarifa hizi ni muhimu jamii kujua -- bila kujulikana wao ni nani. Tor inatumika na wanaharakati duniani kote ambao wanapinga serikani kandanizi na kulinda haki za binadamu, sio tu kwa usalama wao na kutojulikana, lakini pia kukwepa udhibiti wa mtandao ili sauti zao zisikike. Tor inawezesha mamilioni ya watu kujilinda mtandaoni, Haijalishi nafasi walizonazo au wasizonazo. Kwa toleo letu la tatu la PrivChat, tutaleta maisha halisi ya watumiaji wa Tor ambao wataelezea namna Tor imekuwa muhimu kwao na kazi zao katika kulinda haki za binadamu na uhuru duniani kote.

PrivChat na Tor Sura ya #2- Nzuri, Mbaya na Mbaya kwa ukwepaji wa udhibiti

Pamoja na Felicia Anthonio, Vrinda Bhandari, Cecylia Bocovich na Arturo Filastò. Inasimamiwa na Cory Doctorow.

Kila mwaka, udhibiti wa mtandao unaongezeka ulimwenguni.Kutoka katika kiwango cha udhibiti wa mtandao hadi udhibiti wa mtandao kitaifa, serikali na makampuni binafsi wana zana zenye nguvu kuzuia taarifa na mawasiliano kwa watu. Watu wengi, makundi na taasisi wanafanya kazi ya uvumbuzi, kupima na kupambana dhidi ya udhibiti wa mtandao-- na wanawasaidia mamilioni ya watu kujiunganisha na mtandao mara kwa mara na kwa usalama. Licha ya mafanikio hayo, tunapitia changamoto ya kutopata ufadhili mzuri mabilioni ya dola kutumia katika udhibiti na mbinu nyingine zikiendelea. Toleo la pili la PrivChat la Tor linaweza kuhusu uzuri, ubaya unaotokea katika ukwepaji wa udhibiti wa mtandao. Katika dunia ambayo teknolojia ya udhibiti unazidi kuwa wa kisasa na inanunuliwa na kuuzwa katika nchi, hivyo ni ubunifu wetu kupima na kutengeneza dhana za kukwepa udhibiti huo, vilevile na utayari wa watu kupambana na hilo. Lakini je inatosha? Vikwazo gani vinawapata watu na taasisi wanapopambania uhuru wao wa mtandao?

PrivChat na Tor Sura ya #1-faragha ya mtandaoni mwaka 2020: Uharakati na COVID 19

Pamoja na Carmela Troncoso, Daniel Kahn Gillmor na Matt Mitchell. Inasimamiwa na Roger Dingledine.

Ulipottokea mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 nchi nyingi duniani, serikali nyingi ziliangalia teknolojia zinazoweza kuzuia ueneaji wa virusi ili kuukabili ugonjwa huo. Vitendo teknolojia za kufuatilia mawasiliano vimeibua maswalki mengi kuhusiana na faragha, hasa katika: Je inawezekana kukamata kirusi huku tukiheshimu faragha za watu? Sasa kati ya ukinzani nchini Marekani. kinyume na ubaguzi wa rangi, uliofuatwa na wapinzani wengi duniani kote, swali kuu kuhusiana na kufuatilia na kuchukua taarifa za mawasiliano, faragha, na ufuatiliaji mtandaoni vimekuwa muhimu. Teknolijia iliyotumiwa kukamata virusi je inaweza kutumiwa kukamata wapinzani? Itawezekana? Kwa PrivChat yetu ya kwanza, Tor Project inakuletea wageni mashuhuli watatu kuchati nasi kuhusu faragha katika muktadha huu.